Saturday, August 13, 2016

SAKATA LA Hassan Kessy lanoga

Tags



Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeweka bayana majina ya wachezaji ambao waliombewa vibali vya kushiriki katika hatua ya makundi huku likiwepo jina la mlinzi wa zamani wa Simba Hassan Kessy Ramadhani ambaye kwasasa yupo Yanga.
Cloud FM kupitia kipindi chake cha michezo Sports Extra kilifanya mazungumzo na afisa habari wa TFF Alfred Lucas ambaye alitoa ufafanuzi kwanini nyota huyo hashiriki michuano hiyo wakati jina lake lipo kwenye orodha ya majina ya wachezaji wanaotakiwa kucheza mashindano hayo ambayo kwa sasa yanaelekea ukingoni katika hatua ya makundi.
Picha lilivyoanza
Tulipofungua usajili, Yanga walitulea majina manne likiwemo jina la Hassan Kessy, Vicent Andrew ‘Dante’ na Beno Kakolanya na Juma Mahadhi. Baada ya kupeleka yale majina na kwakua tulishasajili tangu tarehe 15 hadi tarehe 8 mwezi August kwamba ndiyo mwisho wa usajili tulipeleka majina na kupokelewa kisha kazi ikafanywa mara moja na CAF kupitisha hayo majina.
Lakini mwisho wa siku wachezaji wote akina Dante, Juma Mahadhi na Kakolanya walikuwa na ruhusa ya kucheza kwasababu walikuwa na barua kutoka vilabu walivyokuwa wanachezea awali (release letter).
Kessy anaweza kucheza dhidi ya MO Bejaia?
Kessy hawezi kucheza mchezo dhidi ya MO Bejaia kwasababu Yanga bado hawajamalizana na Simba, kwa mujibu wa barua yao iliyopo TFF, Simba wanadai Hassan Kessy alivunja mkataba kabla ya wakati.
Kwa mujibu wa mikataba ya usajili ya kitaifa na kimataifa kuanzia January 15 hadi June 15, Kessy alikuwa na nafasi ya kufanya mazungumzo na klabu yoyote kwasababu mkataba wake ulikuwa unaelekea kumalizika. Lakini madai ya Simba kwa mujibu wa barua zao ni kwamba, Hassan Kessy japokuwa alikuwa na ruhusa ya kufanya mazungumzo lakini hakuwa na ruhusa ya kutumikia, kitendo cha kutumikia kinatafrisiriwa na Simba kwamba ni kuvunja mkataba.
Simba wanasemaje?
Simba wanamtuhumu Kessy kwamba alianza kushiriki shughuli za Yanga kabla. Mazoezi na shughuli nyingine ikiwemo ile ya tarehe 25 May siku ya Jumatano kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA ambapo Yanga ilicheza na Azam. Kessy alikuwa upande wa Yanga na mbali na hapo alifanya mazoezi na klabu ya Yanga kwa mujibu wa Simba ikiwa tarehe 15 ya mwezi June bado haijafika (siku ya kumalizika kwa mkataba wake).
Baada ya fainali hiyo Simba wanaendelea kumtuhumu Kessy kuendelea na mazoezi na klabu ya Yanga, wanasema kwamba, kati ya tarehe 12 June siku tatu kabla ya mkataba wake kumalizika, alisafiri na Yanga kwenda Uturuki  ambapo Yanga ikwenda kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za nane bora za kombe la shirikisho.


EmoticonEmoticon