Thursday, August 18, 2016

MAKALA

Tags

KISA CHA AJABU CHA JURAIJI.
Kisa cha Mbani Israil aliyeitwa Juraij kimesimuliwa na Mtume wetu S.A.W. katika Hadithi. Jureij alikuwa ni mtu mchaMungu wa zama hizo aliyejenga hekalu lake kwa udongo kwa ajili ya kufanya ibada. Upande mmoja alikuwa hamjali mama yake. Kwa hivyo mama yake alimuombea apatikane na tatizo la uzinifu. Na dua la mama yake likampata. Na upande mwingine alikuwa ni mtu mchaMungu kupita kiasi. Hivyo Mola wake alimuokoa na janga hilo la tuhuma ya zina. Kisa hiki kimetolewa kwa urefu katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari na Muslim, Mtume S.A.W. kasema, “Maana yake, 

“Hakuna aliyesema uchangani isipokuwa watatu: 
 Issa bin Maryam na 
 (mwingine) ni rafiki wa Juraij. 
Na alikuwa (Mbani Israil) mchaMungu akiabudu kwenye hekalu. (Siku moja) alikuwa humo (hekaluni) akisali akamjia mama yake (kamkumbuka mwanawe Juraij) akamwita:
“Ewe Juraij! (Juraij) akasema (moyoni mwake): 
“Ewe Mola wangu! Mama yangu (ni bora) au Sala yangu, (nifahamishe nimjibu au niendelee kusali?). Akaelekea Sala yake. Mama yake akaondoka. Ilipokuja kesho yake akamjia naye akisali akasema: 
“Ewe Juraij!” (Juraij) akasema (moyoni mwake): 
“Ewe Mola wangu! Mama yangu (ni bora) au Sala yangu (nifahamishe nimjibu au niendelee kusali?). Akaelekea Sala yake. Mama yake akaondoka. Siku ya tatu akamjia naye akisali akasema: 
“Ewe Juraij!” (Juraij) akasema (moyoni mwake): 
“Ewe Mola wangu! Mama yangu (ni bora) au Sala yangu (nifahamishe nimjibu au niendelee kusali?). Akaelekea Sala yake. (Mama yake akaghadhibika) akasema (kwa hamaki): 
“Ewe Allah! Usimfishe (Juraij) mpaka umuoneshe nyuso za wazinifu (malaya).” 
Mabani Israil wakawa wakimzungumzia Juraij na ibada yake. Na alikuwapo mwanamke mzinifu (wa Ki-Bani Israil) akipigiwa mfano kwa uzuri wake. (Mwanamke yule mzinifu) akasema: “Mkitaka mimi nitamfanyia (Juraij) majaribio kwa ajili yenu.” Kasema: “Akenda kujionesha kwake lakini (Juraij) hakumjali.” Akamwendea mchungaji aliyekuwa akiishi katika hekalu la (Juraij) akazini naye akabeba mimba. Alipokwishazaa akasema: “Yeye ni wa Juraij.” 
Wakamjia (Juraij) wakamtoa wakavunja hekalu lake na wakawa wakimpiga. (Juraij) akasema: 
“Mna nini (mbona mnanipiga na mmevunja hekalu langu?)” 
Wakajibu: “Umezini na huyu mwanamke mzinifu akakuzalia (mtoto wa haramu).” 
Akauliza: “Yuko wapi huyo mtoto?” 
Wakamleta. Akasema: “Niacheni (kwanza) mpaka nisali.” Akasali, alipokwisha (sali Sala yake) akamjia mtoto akambinya tumboni mwake akasema: 
“Ewe kijana! Nani baba yako?” 
Akajibu (mtoto): “Mchunga mbuzi fulani.” Kasema: 
“Wakamgeukia Juraij wakimbusu na wakimuomba radhi.” Wakasema: “Tutakujengea hekalu lako kwa dhahabu.” 
Akajibu: “La! Irudisheni kama ilivyokuwa kwa udongo.” Wakajenga.
Mazingatio:
 Ni sala ya faradhi tu inayokuwezesha kutoikata pale mzazi atakapokuwa amekuita, lakini kama unasali sala ya suna basi utalazimika kumwitikia mzazi (kukata swala) pale anapokuita
 Kuenda kunyume na maelekezo (yaliyopo juu) dua ya mzazi inaweza kukupata kama ilivyotokea kwa Juraid
 Kwa kumtii kikweli Allaah, huepushwa na madhara mengi
Waliosema wakiwa bado wachanga
1. Mtotot aliyemtetea kwenye kesi ya kusingiziwa kubaka Nabii Yusuf
2. Nabii Issa
3. Na huyu mtoto wa mchungambuzi aliyesingiziwa Juraid


EmoticonEmoticon