Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ametangaza kamati mpya ya mashindano ambayo imeanza kazi yake mara moja.
“Mwenyekiti amevunja rasmi kamati ya mashindano iliyokuwa chini ya mjumbe wa kamati ya utendaji iliyopita Mhandisi Isack Chanji mara moja kuanzia leo, Mwenyekiti wa Yanga kwa mamlaka aliyonayo ya kuteua wajumbe watatu wa kamati ya utendaji amemteua Mhandisi Paul Malume kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji mpya na pia kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya mashindano mara moja kuanzia sasa” amethibitisha Deusdetith kaimu Katibu mkuu wa Yanga.
Kamati mpya ya mashindano ambayo Mwenyekiti wake ni Paul Malume inaundwa na wajumbe walioteuliwa ambao ni;
- Mustafa Ulungo
- Eng. Mahende Mugaya
- Abdallah Bin Kleb
- Jackson Maagi
- Samwel Lukumay
- Hussein Nyika
- Athumani Kihamia (kutoka Arusha)
- Felix Felician Minde (kutoka Mwanza)
- Leonard Chinganga Bugomola (kutoka Geita)
- Omary Chuma
- Hussein Ndama
- Hamad Ali Islam
- Yusuphed Mhaden
- Beda Tindwa
- Moses Katabalo
- Roger Lamlembe
Kwa maana hiyo, Mhandisi Isack Chanji atabaki kuwa mshauri kamati hiyo mpya ya mashindano.
EmoticonEmoticon