KUHUSU MAANDAMANO YA CHADEMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kufanya maandamano nchi nzima Septemba Mosi kupinga kile inachoeleza kuwa ni kuminywa kwa demokrasia nchini.
Licha ya Jeshi la Polisi kusema kuwa maandamano hayo si halali, chama hicho kimezidi kusisitiza kuwa maandamano hayo yapo pale pale na hakuna wa kuyazuia.
Akiungumzia maandamano hayo Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amesema mazungumzo ya vyama vya siasa yatakayofanyika Agosti 29 na 30 yataamua kuwepo au kutokuwepo maandamano yaliyopangwa kufanywa na CHADEMA Septemba mosi.
Tayari watu kadhaa wamekamatwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na fulana zenye maneno yanayohusu operesheni UKUTA ambayo jeshi hilo limesema kuwa ni maandamano yasiyo halali.
EmoticonEmoticon