Wednesday, August 8, 2018
Thursday, February 23, 2017
TUME YA VYUO VIKUU YATANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI WASIO NA SIFA
Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza zaidi ya majina ya wanafunzi
8,436 kutoka vyuo vya elimu ya juu 52 nchini wasiokuwa na sifa ya
kufanya masomo ya ngazi hiyo.
Sehemu ya taarifa kwa umma ambayo
imewekwa kwenye tovuti ya tume hiyo imesema, "TCU inautangazia umma kuwa
zoezi la uhakiki wa sifa za wanafunzi wanaondelea na masomo kwenye vyuo
vya elimu ya juu nchini kwa mwaka 2016/2017 limekamilika katika baadhi
ya vyuo," liliandika tangazo hilo.Kwa mujibu wa tangazo hilo, majina ya wanafunzi hao wasiokuwa na sifa, wamo hadi waliopo mwaka wa mwisho wa masomo yao.
Taarifa hiyo iliyotolewa Februari 20 na kuwekwa kwenye tovuti ya tume hiyo inasema.
"Katika kutekeleza zoezi hilo tume imebaini kuwa kuna wanafunzi ambao wamedahiliwa katika program ambazo hawana sifa. Orodha ya wanafunzi wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika," inasema sehemu ya taarifa hiyo.
SOKO LA HISA LAZUIA HISA ZA TIGO
Siku
moja baada ya kampuni ya Tigo kuanza kuhaha mitandaoni ikikanusha kuwa
kampuni hiyo haimilikiwi na kampuni ya Golden Globe inayomilikiwa na
mfanyabiashara Yusuf Manji, Nankaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana
(CMSA) imesimamisha mchakato wa kuingiza hisa za Tigo katika Soko la
Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Jana
kulisambaa taarifa mitandaoni, Tigo ikipinga kwamba Tigo inamilikiwa na
Manji. Hii ikiwa ni baada ya vyombo vya habari kueleza mfanyabiashara
huyo alivyonunua kampuni hiyo namba mbili kwa ukubwa kwa zile za
mawasiliano nchini.
Kawaida kampuni hutakiwa kujisajili kwa asilimia 25 ya hisa zake, hii ni kwa mujibu wa sheria.
Hadi
sasa kuna kesi mahakamani, Golden Globe ya Manji ambayo iliinunua
kampuni hiyo ilipopigwa mnada na Milcomn Tanzania NV ambao walikuwa
wamiliki wa awali.
Wednesday, February 22, 2017
WAZIRI WA HABARI NA SANAA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (Mb) kesho Februari 23, 2017 anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa miguu kwa vijana na wanawake.
Uzinduzi huo utakaofanyika saa 5.00 asubuhi, utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo. Utafanyika kwenye Ukumbi wa
Hoteli ya Courtyard, Upanga jijini Dar es Salaam.
Monday, September 5, 2016
Jinsi ya kuandika SMS ijitume
Jinsi Ya Kuandika Meseji Zitakazojituma Zenyewe Baadae
Siku hizi maisha yanakimbia sana na kila kukicha majukumu yanaongezeka kwa kasi ya ajabu, ni rahisi sana kusahau baadhi ya ratiba kama kufanya mawasiliano na watu wako wa muhimu. Hapa ndipo umuhimu wa kuwa na uwezo wa kuset meseji zinazojituma unapokuja.
Sunday, September 4, 2016
Ahadi za Rais Magufuli Zenji
MO Blog imekuandika mambo aliyoyaahidi Rais John Pombe Magufuli wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya Kibanda Maiti kisiwani Unguja ni pamoja na kuifanya Zanzibar kuwa makao makuu ya viwanda vya samaki na hoteli za kitalii.
Kutoka ofisi za CUF
Jeshi la Polisi limelazimika kufyatua risasi angani na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba waliokuwa wakimzuia mwenyekiti wa muda wa CUF, Julius Mtatiro, kuingia ofisini eneo la Buguruni.
Saturday, September 3, 2016
Kampuni ya Acer
Kampuni ya Acer ya nchini Taiwan, imeweke rekodi baada ya kuzindua Laptop ya kwanza (Predator 21X) yenye kioo chenye mikunjo (curved).
Kampuni ya Acer
Kampuni ya Acer ya nchini Taiwan, imeweke rekodi baada ya kuzindua Laptop ya kwanza (Predator 21X) yenye kioo chenye mikunjo (curved).
Tuesday, August 30, 2016
How to Secretly Turn Off Your Android Device By sending A Single Text Message
How to Secretly Turn Off Your Android Device By sending A Single Text Message
With This Text Message Bypass Android Lock Screen Without Data Loss
With This Text Message Bypass Android Lock Screen Without Data Loss
Note: This Trick may or may not work on some device. We have personally tested this and it works fine for us.
Monday, August 29, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)