Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kibiti, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Peter Kubezya aliyeuwawa na watu wanaoaminika huenda ni magaidi, alikuwa shabiki mkubwa wa Yanga.
Marehemu Kubezya alikuwa kati ya mashabiki wakubwa wa Yanga ambao ndiyo mabingwa watetezi wa Tanzania Bara.
Askari huyo aliuwawa katika opresheni maalum aliyokuwa akiiongoza katika enero Jaribu Mpakani wilayani Kibiti.
Tukio
lilitokea katika kizuizi cha barabarani katika eneo hilo na aliwawa
wakati wa majibizano na askari hao baada ya kupigwa risasi kiunoni.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, Boniventure Mushongi
alithibitisha kifo cha Kubezya ambaye hivi karibuni alihitimu elimu ya
chuo kikuu.
Mwenyezi Mungu Amrehemu.
23
Feb
2017
EmoticonEmoticon