Jeshi la Polisi limelazimika kufyatua risasi angani na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba waliokuwa wakimzuia mwenyekiti wa muda wa CUF, Julius Mtatiro, kuingia ofisini eneo la Buguruni.
Itakumbukwa hivi karibuni CUF kilimteua Julius Sunday Mtatiro kuwa mwenyekiti wa muda baada ya mwenyekiti aliyekuwepo, Prof. Lipumba kijiuzulu Agosti 2015.
Julius Mtatiro jana alitangaza kufanya mkutano na waandishi wa habari leo katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam ili kuzungumzia kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa visiwani Zanzibar
EmoticonEmoticon