Thursday, February 23, 2017

TUME YA VYUO VIKUU YATANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI WASIO NA SIFA

Tags


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza zaidi ya majina ya wanafunzi 8,436 kutoka vyuo vya elimu ya juu 52 nchini wasiokuwa na sifa ya kufanya masomo ya ngazi hiyo.
Sehemu ya taarifa kwa umma ambayo imewekwa kwenye tovuti ya tume hiyo imesema, "TCU inautangazia umma kuwa zoezi la uhakiki wa sifa za wanafunzi wanaondelea na masomo kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini kwa mwaka 2016/2017 limekamilika katika baadhi ya vyuo," liliandika tangazo hilo.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, majina ya wanafunzi hao wasiokuwa na sifa, wamo hadi waliopo mwaka wa mwisho wa masomo yao.
Taarifa hiyo iliyotolewa Februari 20 na kuwekwa kwenye tovuti ya tume hiyo inasema.
"Katika kutekeleza zoezi hilo tume imebaini kuwa kuna wanafunzi ambao wamedahiliwa katika program ambazo hawana sifa. Orodha ya wanafunzi wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Wema Sepetu mahakamani tena

Tags
wema sepetu amsindikiza Mbowe mahakamani

SOKO LA HISA LAZUIA HISA ZA TIGO

Tags
 
Siku moja baada ya kampuni ya Tigo kuanza kuhaha mitandaoni ikikanusha kuwa kampuni hiyo haimilikiwi na kampuni ya Golden Globe inayomilikiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji, Nankaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imesimamisha mchakato wa kuingiza hisa za Tigo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Jana kulisambaa taarifa mitandaoni, Tigo ikipinga kwamba Tigo inamilikiwa na Manji. Hii ikiwa ni baada ya vyombo vya habari kueleza mfanyabiashara huyo alivyonunua kampuni hiyo namba mbili kwa ukubwa kwa zile za mawasiliano nchini.

Kawaida kampuni hutakiwa kujisajili kwa asilimia 25 ya hisa zake, hii ni kwa mujibu wa sheria.

Hadi sasa kuna kesi mahakamani, Golden Globe ya Manji ambayo iliinunua kampuni hiyo ilipopigwa mnada na Milcomn Tanzania NV ambao walikuwa wamiliki wa awali.



OFISA WA POLISI ALIYE UWAWA

Tags
 

Wednesday, February 22, 2017

KIUNGO WA ZAMANI WA GHANA AJIUNGA NA THOMASI ULIMWENGU

Tags

Tags
  WAZIRI WA HABARI NA SANAA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (Mb) kesho Februari 23, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa miguu kwa vijana na wanawake.


Uzinduzi huo utakaofanyika saa 5.00 asubuhi, utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo. Utafanyika kwenye Ukumbi wa 
Hoteli ya Courtyard, Upanga jijini Dar es Salaam.